Athari Za Lugha Ya Kijinsia Katika Kusuluhisha Changamoto Za Kiekolojia Katika Riwaya Ya Nakuruto (2009) Ya Clara Momanyi

Authors

DOI:

https://doi.org/10.51317/eajk.v5i1.1175

Keywords:

Ekolojia, fasihi, jinsia, lugha, mabadiliko

Abstract

Swahili

Makala hii inalenga kutathmini athari za lugha ya kijinsia katika kusuluhisha changamoto za kiekolojia katika riwaya ya Nakuruto (2009) ya Clara Momanyi. Mabadiliko ya ekolojia yameathiri binadamu kutokana na matukio makali ya hali ya anga yanayoletwa na mabadiliko ya tabianchi. Mabadiliko ya ekolojia yamkini yanaonekana kuwa na athari tofauti kwa namna jinsia hizi zinavyokabiliana na kutekeleza majukumu husika. Ingawa taaluma nyingi zinaendelea kutafuta suluhisho la athari za mabadiliko ya ekolojia, ni wazi kuwa suluhisho kamili halijapatikana. Fasihi haijabaki nyuma katika utoaji wa mchango wake kuhusu ekolojia. Hata hivyo, tafiti chache tu ndizo zimejaribu kuhusisha fasihi na ekolojia huku zikilenga mtazamo wa mwandishi au jinsia ya kike pekee katika uchanganuzi wa makala mbalimbali za fasihi. Kwa hivyo, kuna haja ya kuangazia jinsia zote za kike na kiume katika utafutaji wa suluhisho kuhusu mabadiliko ya tabianchi. Utafiti huu ulielekezwa na lengo mahususi la kutathmini athari za lugha ya kijinsia katika kusuluhisha changamoto za kiekolojia katika riwaya ya Nakuruto. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Ekofeministi na ulitumia muundo wa kiuchanganuzi. Usampulishaji dhamirifu wa kivigezo ulitumika kupata data za kimsingi kutoka kwa watoa taarifa kupitia usaili na data za sekondari kutoka katika riwaya ya Nakuruto. Orodhahakiki na dodoso zilitumika kama vifaa vya ukusanyaji wa data. Data zilichanganuliwa kulingana na lengo la utafiti na kuwasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Utafiti ulibaini kuwa jinsia zote zina nafasi sawa katika kuleta suluhisho kwa changamoto za kiekolojia. Utafiti huu ulibainisha kuwa taaluma ya fasihi ina jukumu la kuwasilisha suluhisho kwa changamoto zinazosababishwa na mabadiliko ya ekolojia. Pia ulichangia mijadala ya uhakiki wa matumizi ya lugha kijinsia kuhusu masuala ya ekolojia.

English

This article evaluates the effects of gendered language in addressing ecological challenges in Clara Momanyi’s novel Nakuruto (2009). Ecological change continues to affect humanity through extreme weather conditions associated with climate change. However, because of differentiated gender roles in society, ecological changes tend to have different impacts on men and women as they undertake their socially ascribed roles. Although other disciplines have attempted to find solutions to the impacts of ecological changes, comprehensive solutions have yet to be achieved. Literature has therefore also engaged in seeking remedies to the impacts of ecological changes. However, only a few studies have examined ecological literature, and existing studies have largely focused on the author’s perspective and that of the female gender in the analysis of literary texts. Therefore, there is a need to involve both female and male genders in seeking solutions to ecological challenges. The study was guided by Ecocriticism Theory and employed an analytical research design. The study found that all genders have an equal role in addressing ecological challenges. The study contributes to understanding the role of literature in addressing ecological challenges and their mitigating factors. In addition, it contributes to critical debates on the use of gendered language in ecological contexts.

 Keywords: Change, ecology, gender, language, literature.

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2026-09-10

Issue

Section

Articles

How to Cite

Athari Za Lugha Ya Kijinsia Katika Kusuluhisha Changamoto Za Kiekolojia Katika Riwaya Ya Nakuruto (2009) Ya Clara Momanyi. (2026). Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK), 5(1), 144-151. https://doi.org/10.51317/eajk.v5i1.1175

Similar Articles

1-10 of 33

You may also start an advanced similarity search for this article.